Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza Arafi, Mudir wa Hawza nchini Iran, ametoa taarifa akilaani vikali shambulio la anga lililofanywa na Marekani dhidi ya maeneo ya makazi na sherehe ya harusi katika eneo la Sirik, lililopo katika mkoa wa Hormozgan.
Maandishi ya taarifa hiyo ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
«“Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa.”
(Al-Israa, Aya ya 33)»
Kwa mara nyingine tena, sura mbaya na ya kuchukiza pamoja na tabia ya kinyama dhidi ya ubinadamu ya mfumo wa utawala wa mabavu na ubeberu wa kimataifa, hususan utawala wa Marekani unaofanya uchokozi, vimejitokeza wazi kupitia uhalifu huu wa kikatili.
Shambulio la anga lililofanywa mapema leo alfajiri dhidi ya maeneo ya makazi na sherehe ya harusi katika eneo la Sirik, lililopo katika mkoa wa Hormozgan, ambalo limesababisha kuuawa kishahidi na kujeruhiwa kwa raia kadhaa wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto wasio na hatia, limeweka wazi zaidi ukubwa wa kutisha wa uchokozi huu wa kinyama na usio wa haki.
Uhalifu huu, ukiwa ni mwendelezo wa kuvunjwa Makubaliano ya Islamabad na mfululizo wa mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na wanajeshi wa Marekani dhidi ya wananchi wanyonge wa Iran, yakiwemo kulipuliwa kwa Shule ya Shajareh Tayyibeh ya Minab na kuuawa kishahidi makumi ya wanafunzi, pamoja na kushambuliwa Uwanja wa Michezo wa Lamerd, hospitali na maeneo ya kiraia, umethibitisha tena kwamba ugaidi wa dola ya Marekani hautambui mipaka yoyote na kwamba usalama na maisha ya watu wasio na hatia havina thamani yoyote machoni mwao.
Ukimya wa aibu wa wale wanaodai kwa uongo kutetea haki za binadamu, pamoja na mashirika ya kimataifa, mbele ya majanga haya, unastahili kutafakariwa na kuhojiwa.
Maadui wenye chuki kubwa na wajue kwamba Iran yenye fahari, Mhimili wa Muqawama, pamoja na taasisi zote za kijeshi na kiraia, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, zitasimama imara dhidi ya uchokozi unaoelekezwa dhidi ya Uislamu, Iran na Umma wa Kiislamu.
Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa baraka na msaada wa Walii wa Zama (aj), watafungua ukurasa mpya na kuweka mfano mpya wa Muqawama dhidi ya utawala wa mabavu wa kimataifa na kishetani, na watachora hatua mpya yenye umuhimu mkubwa wa kistaarabu katika mizani na mahusiano ya kikanda na kimataifa.
Kituo cha Usimamizi na taasisi za juu za Hawza, pamoja na wanazuoni na wanafunzi wote wa Hawza tukufu, huku tukitoa pole kwa ajili ya kuuawa kishahidi baadhi ya wananchi wenzetu, na kumuomba Mwenyezi Mungu awaponye waliojeruhiwa na waliopata ulemavu kutokana na tukio hilo, tunalaani vikali kitendo hiki cha kinyama ambacho kinapingana na misingi yote ya kimataifa na kanuni za kibinadamu.
Tunakitambua kitendo hiki kuwa ni mfano wa wazi wa “ugaidi wa dola” na uhalifu wa kivita. Aidha, huku tukiviunga mkono vikosi madhubuti vya kijeshi vya Jamhuri ya Kiislamu, tunaviomba, kwa kufuata amri ya Amiri Mkuu wa Vikosi Vyote vya Jamhuri ya Kiislamu, viendelee kutoa majibu yenye kuleta majuto kwa adui hadi kufikiwa kiwango kamili cha kuzuia uchokozi, na kuongeza zaidi nguvu na nafasi ya Mhimili wa Muqawama wa Kiislamu na Umma wa Kiislamu.
“Na ushindi hautoki isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mwenye Hikima.”
Alireza Arafi
Mkuu wa Hawzah nchini Iran.
Maoni yako